Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametoa wito kwa Baraza la Vyombo vya Habari nchini na wadhibiti wengine kuwaondoa watu wasio na ujuzi katika taaluma ya uandishi wa habari.

Kulingana na Kindiki, matapeli wamefanya kuwa vigumu kwa mashirika ya usalama kutoa ulinzi kwa wanahabari mtandaoni na nje ya mtandao akidai ugumu wa kumtofautisha mwandishi wa habari halisi na mhalifu umesababisha kuwepo kwa matukio mengi ya utapeli.

Aidha aliwahakikishia wanahabari kwamba vyombo vya usalama vitashirikiana na wanahabari kusaidia kulinda uhuru na uadilifu wa vyombo vya habari nchini.

Hali kadhalika aliwataka waandishi wa habari kusimama kwenye ukweli kila wakati.

May 3, 2023