Mdhibiti wa Bajeti nchini Margaret Nyakang’o ameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni 2 na chaguo la mdhamini wa kiwango sawia au dhamana ya shilingi 500,000 pesa taslimu.

Nyakang’o anayeshtakiwa pamoja na watu wengine 10 alikamatwa asubuhi ya leo mjini Mombasa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuendesha chama cha Ushirika bila ya leseni, kughushi nyaraka na pia njama ya kuwalaghai watu mwaka wa 2016 kabla yake kutwaa hatamu za kuwa mdhibiti wa bajeti nchini.

Mdhibiti huyo wa bajeti aidha amekuwa katika vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, baada ya kufichua kwamba mshahara wake umekuwa ukizidishwa mara kadhaa kwa njia isiyoeleweka. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 13 mwezi huu.

December 5, 2023