By Isaya Burugu,Oct 08,2022-Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameagiza kubuniwa kwa kamati ya maswala ya uchukuzi itakayojumuisha wahusika mbali mbali wa sekta hiyo itakayosimamia mikakati ya kupanga mipango ya kukabili tatizo la msongamano wa magari katikati mwa jiji.
Sakaja amehoji kuwa mashirika mbali mbali yanayoshughulikia uchukuzi na udhibiti ya msongamano yamekuwa yakifanya kazi kila moja kivyake na wakati umefika kwa mashairika hayo kufanya kazi Pamoja ili kuleta mwelekeo jijini .
Amesema kaunti zingine nne zinazojumuisha eneo la Nairobi za Kajiado.Kiambu ,Machakos,na Muranga tayari zimebuni kamati yao ya uchukuzi.Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya NTSA George Njao aliyekuwa kwenye mkutano huo ameunga mkono hoja ya kuwa na kamati moja ya uchukuzi wa Nairobi.