Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, ambaye anatazamiwa kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) atapigwa msasa na Bunge Jumanne wiki ijayo.
Wakenya wana hadi Jumatatu wiki ijayo kuwasilisha maoni yao kuhus kuteuliwa kwa Haji kama bosi wa NIS.
Aidha Kuteuliwa kwake na Rais William Ruto wiki jana kumekabiliwa na upinzani kutoka kwa mashirika ya Kiraia ambayo hayana imani naye.
Wanadai Haji ambaye anarejea katika Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi baada ya miaka 6 ya kuhudumu kama DPP alikiuka katiba kwa kuondoa kesi za ufisadi zinazohusisha maafisa wakuu serikalini.