BY ISAYA BURUGU,29TH SEPT,2023-Mkuu wa utumishi wa ummma Felix Kosgey hivi leo amekutana na maafisa wakuu wa usalama.Mkutano huo unaofanyika huko Kabete katika kaunti ya Kiambu unajadili kati ya mengine kuboreshwa kwa mazingira ya utenda kazi kwa maafisa wa usalama nchini bali na kuimarishwa kwa usalama.
Akizungumza katika mkutano huo,Kosgey amesema serikali inatambua jukumu muhimu linalotekelezwa na polisi katika kulinda mipaka ya nchi na iko tayari kufanya kila juhudi kuimarisha utenda kazi wao.Mkuu huyo wa utumishi wa umma vilevile amesema kuwa utoaji mafunzo kwa polisi katika kuboresha utenda kazi wao utaendelea .
Pia ameguzia hatua ya kenya kutuma maafisa wake wa usalama nchini Haiti kukabili makundi ya kigaidi nchini humo kuwa yajivunia na ishara bora kuwa maafisa wa usalama wa taiafa hili wamefikia viwango vya kimataiafa.
Kosgey hata hivyo amezidi kuwakumbusha maafisa hao kuwa wakenya wangali na Imani kwao na kuwategemea kuwalinda na kuwakumnbusha kuwa picha yao machoni mwa wananchi ni ya kutiliwa shaka nani sharti wajizatiti kutenda kazi zao kwa uadilifu na maadili ya hali ya juuu.