BY ISAYA BURUGU,13TH MARCH,2023-Aliyekuwa makamu wa rais wat isa nchini  Moody Awori  amewataka wanasiasa  kuachana na vita vya ubabe wa kivita  na kuunga mkono  utawala war ais  William Ruto ili uweze kutekeleza manifesto yake.Akizungumza baada ya mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi  kumtembelea nyumbani kwake jijini Nairobi, Awori mwenye umri wa miaka 94  amesema wanasiasa  wanapasw akuwa katika mstari wa mbele kuwaunganisha wakenya.

Matamshi yake  yanakuja wakati  kinara wa upinzani Raila Odinga  anafanya  mikutano yakitaifa  kuwaraia wafausi wake  kukatalia mbali utawala wa Ruto.Odinga aliyepoteza kwa Ruto katika uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana, anasisitiza kuwa zoezi hilo lilibiwa  na amekuwa akiuta utawala wa Ruto kama usiokuwa halali.

Kwa mjibu wa Awori Ruto anahitaji heshima , na ungwaji mkono kutoka kwa kila mkenya  anapoongoiza nchi.

 

 

 

 

 

 

March 13, 2023