Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umesisitiza kuwa mpango wa kufanya maandamano dhidi ya serikali kuanzia Jumatano hadi Ijumaa ungali unaendelea licha ya onyo kali kutoka kwa serikali.

Akiongea katika afisi za Wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga (JOOF) Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi alisema kuwa hawataogopa kutekeleza majukumu yao ya kikatiba ya kufanya maandamano ya amani.

Mbunge huyo wa Ugunja alitetea kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwazuia kufanya maandamano yaliyopangwa, awe Rais William Ruto au taasisi yoyote.

Wakati uo huo, alisema kuwa harakati za kukusanya saini za kumtimua Rais Ruto bado ziko mkondoni na zitafanyika sawia na maandamano hayo.

July 17, 2023