Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameahidi kuwa wakenya hawatakua na haja ya kuhofu kuhusu kufurushwa makwao kiholela au kubomolewa makaazi yao nyakati za usiku.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa shule ya Komarok jijini Nairobi alikoandamana na Rais William Ruto, Gachagua amesema kwamba serikali ya Rais William Ruto imetoa ilani kwa viongozi wote watakaotekeleza maagizo yoyote ya kuwafurusha wananchi kutoka kwa makaazi yao pasi na kujadiliana na idara za usalama katika kaunti husika. Naibu wa rais amesisitiza wakenya watakao furushwa kutoka katika ardhi ambayo si yao watapata maeneo mbadala watakapoishi.
SAUTI: Kauli ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua
Katika hafla hiyo aidha, Rais William Ruto aliahidi kuwa wizara ya ardhi imeanzisha juhudi za kutoa zaidi ya hatimiliki 4000 za shamba kwa wakaazi katika kaunti ya Nairobi, kama mojawapo ya njia za kukabiliana na matatizo yanayoibuka kuhusu ardhi katika kaunti hiyo pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo bila hofu.
Soma Pia
- Mawaziri Wateule Ruku na Cheptumo Kupigwa Msasa na Bunge Aprili 14 April 4, 2025
- Mahakama ya Katiba Korea Kusini Yathibitisha Kuondolewa kwa Rais Yoon Suk Yeol April 4, 2025
- Justin Muturi atetea utendakazi wake. April 2, 2025
- Rais Ruto: Mvutano wa Ndani Ulisababisha Kubanduliwa kwa Gachagua April 1, 2025
- Msemaji wa serikali Isaac Mwaura nchini azuru soko la Suswa, Narok mashariki. March 27, 2025