BY ISAYA BURUGU 24TH AUG 2023-Mtandao wa kijamii unaotumia video fupi kupitisha maudhui wa Tiktok utafanya kazi na Kenya katika  mchakato wa kutekeleza mageuzi na kufuatilia maswala yanayochapishwa  na wakenya katika mtandao huo.Hatua hiyo ,kwa mjibu war ais Wiliam Ruto itahakikisha kuwa yanayochapishwa  kwenye jukwaa hilo na wakenya yanafuata miongozo iliyokubaliwa.

Rais Ruto kwenye mkutano wa njia ya video na mkurugenzi mkuu wa Tiktok Shou Zi Chew viongozi hao wamekubaliana kuwa watahakikisha kuwa yanayochapishwa kwenye mtandao huo yanafaa kwa kila mwanajamii.

Hatua hiyo inamanisha kuwa iwapo mmoja atachapishwa maswala yasiyofaa katika mtandao huo ,yataweza kuondolewa mara moja.Wakati  wa mkutano huo Chew pia alikubali kuanzisha afisi ya  Tikotok humu nchini ili kusaidia katika kutekeleza oparesheni zake katika bara la Afrika.Ameahidi kuwajiri wakenya Zaidi kufanya kazi katika jukwa hilo.

 

 

August 24, 2023