Mtandao wa kijamii unaotumia video fupi kupitisha maudhui wa Tiktok utafanya kazi na Kenya katikaΒ  mchakato wa kutekeleza mageuzi na kufuatilia maswala yanayochapishwa na wakenya katika mtandao huo.

Hatua hiyo ,kwa mjibu wa rais Wiliam Ruto itahakikisha kuwa yanayochapishwaΒ  kwenye jukwaa hilo na wakenya yanafuata miongozo iliyokubaliwa.

Rais Ruto kwenye mkutano wa njia ya video na mkurugenzi mkuu wa Tiktok Shou Zi Chew wamekubaliana kuwa watahakikisha yanayochapishwa kwenye mtandao huo yanafaa kwa kila mwanajamii.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa iwapo mmoja atachapisha maswala yasiyofaa katika mtandao huo yataweza kuondolewa mara moja.

WakatiΒ  wa mkutano huo Chew pia alikubali kuanzisha afisi yaΒ  Tikotok humu nchini ili kusaidia katika kutekeleza oparesheni zake katika bara la Afrika.Ameahidi kuwaajiri wakenya Zaidi kufanya kazi katika jukwa hilo.

August 24, 2023