BY ISAYA BURUGU 10TH JULY 2023-Mtoto wa miaka tisa amefariki katika ajali ya barabarani usiku wa kuamkia leo katika eneo la ngata katika Barabara kuu ya Nakuru kuelekea Kisumu.

Watu wengine wanane wamepata majeraha na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Maafisa wa polisi Nakuru magharibi mjini wanamzuilia dereva wa lori linaloaminika kusababisha ajali hiyo.Mabaki ya magari husika yamepelekwa katika kituo cha polisi cha Kaptembwa.

Ajali hiyo imetokea mwendo was aa tatu unusu za usiku wa kuamkia leo.Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Nakuru Magharibi Francis Wahome amedhibitisha kisa hicho.

 

 

 

 

 

July 10, 2023