Mtu mmoja ameaga dunia baada ya kupigwa risasi huku afisa mmoja wa polisi akiachwa na majereha mabaya shingoni kufuatia maandamano katika eneo la Duka moja baada ya Kondoo kugongwa na Trela usiku wa kuamkia leo.
Maafisa wa polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kuwatanya waandamanaji ambao waliwasha moto na kuweka vikingi vya stima katikati ya barabara hatua iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara kuu ya Narok-bomet.
Kulingana na wasafiri ambao wamejipata kwenye msangamano huo, wametoa wito wa suluhu kutafutwa ili kuruhusu watumiaji wa barabara hiyo kuendelea na safari yao.