BY ISAYA BURUGU 28TH DEC 2022-Mtu mmoja ameaga dunia leo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya modern coast kuanguka mtoni kaunti ya Kisii.
Basi hilo liliripotiwa kupoteza mwelekeo na kuacha barabara eneo la Masosa kabla ya kuanguka kwenye mto Nyakomisaro hivi leo asubuhi.
OCPD wa Kisii Central Amos Ambasa amedhibitisha kisa hicho na kusem akuwa mtu mmoja aliifariki katika ajali hiyo na ambaye alikuwa mtembeaji kwa miguu aliyegongwa na basi hilo baada yake kupoteza mwelekeo.
Amesema walionusurika wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kisii ambapo wanaendelea kutibiwa.Basi hilo pia limeondolewa kutoka mtoni na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kisii.Mwili wa aliyefariki umehamishiwa katika hifadhi ya miili ya hospitali ya rufaa ya Kisii.