BY ISAYA BURUGU 29TH NOV 2023-Mkutano wa wabunge waliocchaguliwa kwa tiketi ya vyama vinavyounda mungano wa Azimio la Umoja one Kenya umeidhinisha ripoti ya kamati ya mazungumzo yakitaiafa iliyongozwa na Kimani Ichungwah na Kalonzo Musyoka.

Kinara wa Azimio Raila Odinga ameielezea ripoti hiyo kama isiyokamilifu lakini nzuri . Ameongeza kuwa upinzani umeridhia baadhi ya maswala yaliyoshughulikiwa katika ripoti hiyo yakiwemo haki ya uchaguzi,  kuunda upya tume ya uchaguzi IEBC,Kuongezwa kwa muda wa Mahakama ya Juu kusikiliza na kuamua ombi la uchaguzi wa urais kutoka siku 14 hadi 21,Uhamisho wa majukumu yote yaliyogatuliwa na rasilimali zinazohitajika kwa serikali za kaunti,

Kurekebisha Katiba ili kutoa mgao sawa kwa Serikali za Kaunti kwa si chini ya asilimia 20 ya mapato yote yanayokusanywa na Serikali ya Kitaifa kutoka asilimia 15 ya sasa na  Kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Kata

Hata hivyo kuhusu kubuni wadhifa wa waziri mkuu na ule wa kiongozi rasmi wa upinzani sharti wakenya washiriki kura ya maamuzi.WanaAzimio pia wamelezea kutoridhishwa kwao na kupuuzwa kwa swala la hali ngumu yakimaisha inayowakumba wakenya.

 

 

November 29, 2023