Baraza la Muungano wa Azimio la Umoja limetoa muda wa siku 30 kwa mazungumzo ya pande mbili kukamilika baada ya kuanza.

Mkuu wa Azimio Raila Odinga na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka walisema mazungumzo yao na mrengo wa Kenya Kwanza yatahusu masuala manne pekee ambayo wamekuwa wakiibua wakati wa maandamano.

Baada ya kikao cha majumuisho na kamati yake ya pande mbili mnamo Alhamisi, baraza hilo lilisema halitasita kuchukua hatua mbadala kwa dalili yoyote ya ukosefu wa nia njema kutoka kwa upande wa Kenya Kwanza.

Waliongeza kuwa muungano huo utaendelea kuwashirikisha na kuwaelimisha Wakenya kupitia mikutano ya mijini.

Pia walishikilia kuwa hawatafuti mpango wa kugawana madaraka na serikali, wakitaka kuachiliwa bila masharti kwa watu waliokamatwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.

 

May 4, 2023