BY ISAYA BURUGU,23TH NOV 2023-Waziri wa elimu Ezekiel Machogu ametanagza rasmi Matokeo ya mtihani wa Cheti cha Elimu ya Msingi ya 2023 (KCPE) hivi leo. Mtahiniwa bora zaidi katika mitihani huo  wa mwaka huu  alikuwa na wastani wa alama 428.Kulingana na CS, watahiniwa 8,525 walipata alama 400 na zaidi huku 352,782 wakipata zaidi ya 300.

Machogu alisema kuwa watahiniwa 658,278 walikuwa na alama 200 na zaidi wakiwa 383, 025 walipata zaidi ya alama 100.Takriban watahiniwa 1,406, 559 walifanya mitihani yao ya KCPE na takriban milioni 1.2 walifanya mitihani ya KPSEA (Daraja la 6) kati ya Oktoba 30 na Novemba 1, kuashiria mwisho wa mfumo wa elimu wa 8-4-4 katika shule za msingi.

Kwenye matokeo hayo,Watahiniwa 8,523 walipata zaidi ya alama 400 huku watahiniwa 352,782 wakiwa na kati ya alama 300 na 399

Bano la 200-299 lilikuwa na watahiniwa wengi zaidi wakiwa 658,278, huku wengine 38,3025 wakipata kati ya alama 100 na 199.

Wale walio na alama chini ya 99 walikuwa 260. Ili kupata  matokeo kwenye simu zao watanaiwa wanatakiwa  kutuma nambari yao ya usajili  ikifuatiwa na neno KCPE kwa nambari 40054.Ujumbe huo utagharimu shilingi  25.

 

November 23, 2023