BY ISAYA BURUGU 25TH APRIL,2023-Mwanamke wa miaka 27 katika mtaa wa Milimani kule kitengela kaunti ya Kajiado amemdunga kisu na kumua mtoto wake wa umri wa miaka miwili na baadaye kula mwili wa mtoto huyo
.Majirani wamesema kuwa Olivia Naserian alijifungia ndani ya nyumba na alikuwa akicheza na mtoto kabla ya kugeuka na kuzua fujo huku akiharibu vyombo vya nyumba .Kelele kutoka kwa vyombo vilivyokuwa vikivunjwa iliwavutia majirani waliofika na kushuhudia Naserian akimdunga kisu mtoto huyo kwa jina Gloria Njeri mara kadhaa kwani hawangeweza kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa imefungwa.
Majirani waliwapasha polisi Habari walioweza kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba na kumpata mshukiwa akiwa amepoteza fahamu.Akidhibitisha kisa hicho OCS wa Kitengela David Shani amesema kuwa mwanamke huyo alimkata mtoto huyo vipande vipande na kula matumbo yake Pamoja na figo.
Mwanamke huyo alipelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kitengela kwa matibabu na kulazimishwa kutabika vipande hivyo vya mwili ambavyo vitatumiwa kama Ushahidi.Majirani wanadai kuwa mwanamke huyo alimuua mwanawe baada ya kudaiwa kuachana na mumewe.