BY ISAYA BURUGU 25TH APRIL,2023-Mahakama kuu ya  Kajiado imeagiza mwanamke anayekumbwa na makosa ya kumua mwanawe wa miaka miwili  kwa kukata kata mwili wake vipande vipande na kisha kula matumbo yake azuiliwe kwa siku kumi .

Olivia Naserian anatuhumiwa kumua bintiye Gloria Njeri nyumbani kwao mtaani milimani huko Kitengela mnamo jumapili na kula baadhi ya sehemu za mwili wake  kabla ya majirani kuwapasha polisi habari waliofika eneo la tukio na kumtia nguvuni.

Mtuhumiwa amefika mbele ya hakimu mkuu Jane Kamau aliyeagiza kuwa  Naserian asalie kizuizini kwa siku kumi Zaidi  ili kuwaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi.Naserian anatarajiwa kurejea tena mahakamani tarehe 8 mwezi ujao wa Mei siku ambayo kesi hiyo itasilikizwa.

Wakati huo huo mwili wa mwanawe umehamishiwa katika makafani ya hopsitali ya Kitengela.

April 25, 2023