BY ISAYA BURUGU,29TH APRIL,2023-Wakaazi wa Kijiji cha Kibunja,kaunti ndogo ya  Molo kaunti ya Nakuru wameachwa na mshangao baada ya mwanamke mmoja kupatikana akishikilia mwili wa mumewe kwa Zaidi ya waki moja baada yake kuaga dunia.

Inashukiwa kuwa mwanamme huyo alifariki dunia Zaidi ya wiki moja iliyopita kabla ya wmwili wake kugunduliwa ukilala kitandani ambapo mkewe anaminika kuwa amekuwa akilala pia. Wakaazi wanadai kuwa waliamua kuulizia  aliko mwanamme huyo baada yake kutoweka kwa muda.

Hapo ndipo mwili wa mwanamme huyo uliokuwa tayari umeanza kuoza ulipopatika nyumbani mwake jana jioni.

Kis ahicho kilidhibitishwa na naibu chifu wa eneo hiloEvans Oketch aliyewataka wakaazi kuishi vyema na majirani zao.Mwili huo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ndogo ya molo huku uchunguzi ukianzishwa.

 

April 29, 2023