Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 40 alifikishwa katika mahakama ya Narok baada ya kupatikana na kilo 170 ya nyama ya punda milia.
Konene sordo ambaye aliwasilishwa mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama hiyo phyllis shinyanda, alikiri kuwa alipatikana na nyama hiyo aliyokuwa akiisafirisha kwa kutumia piki piki baada ya kupakia katika vijikaratasi 3. Sordo alikamatwa na maafisa wa shirika la kuwalinda wanyamapori la KWS katika eneo la supetai tarehe 10 mwezi huu, katika kaunti ndogo ya Narok kusini pamoja na wanaume wengine wawili ambao hawakuwa mahakamani.
Mwanaume huyo aliiomba mahakama kumwachilia kwa dhamana ili akatafute matibabu aliyouguza baada ya kuanguka na piki piki hiyo alipokuwa anajaribu kuhepa maafisa hao wa kws wasimkamate. Upande wa mashtaka hata hivyo ulipinga ombi hilo, ukisema kwamba kuachiliwa kwake kutaadhiri uchunguzi unaoendelea,
Hata hivyo hakimu aliagiza maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa mshukiwa anapokea matibabu na kuendelea kuzuiliwa, huku Kesi yenyewe ikitarajiwa kutajwa tena tarehe 23 mwezi huu.