Mwanaume mwenye umri wa miaka 50 kutoka eneo la Entasekera Narok Kusini amekiri kosa la kumwoa msichana mwenye umri wa miaka 9 na kukubali mashtaka dhidi yake katika kesi iliyowasilishwa mbele ya hakimu mkazi Phyllis Shinyada mchana wa leo.
Mwanaume huyo kwa jina Saigilu Ololosereka, aliiambia mahakama kwamba alipewa msichana huyo na baba mzazi wa msichana ili aweze kumwoa.
Afisa wa maswala ya watoto katika kaunti ya Narok Pilot Khaemba aliiambia mahakama kuwa ndoa hiyo iligunduliwa baada ya mtoto huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 12, kupata matatizo wakati wa kujifungua na kulazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Narok kwa matibabu.
Inaarifiwa kwamba muuguzi mmoja katika hospitali ya rufaa ya Narok aliwajulisha maafisa wa polisi kuhusiana na kisa hicho msichana huyo alipofikishwa hospitalini kujifungua. Msichana huyo alilazimishwa kuingia kwenye ndoa ya mapema na babake baada ya kupashwa tohara akiwa na umri wa miaka saba.
Juhudi za kumfanyia upasuaji wakati wa kujifungua pia hazikuzaa matunda kwani mtoto mwenyewe aliaga wakati wa kuzaliwa. Afisa Khaemba pia aliiomba kibali cha kumhifadhi msichana huyo katika makao ya watoto ya Taraja huko Machakos pindi atakapotoka hospitalini, Ombi lao lilikubaliwa na mahakama.Taarifa za
Mahakama iliamuru mzee huyo kuzuiliwa na polisi hadi Januari 11, hukumu itakapotolewa.