BY ISAYA BURUGU,4TH APRIL,2023-Polisi katika Kaunti Ndogo ya Manga, kaunti ya Nyamira wanachunguza kisa ambapo mwili wa mtoto wa miaka 11 wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ekoro, kaunti ndogo ya Nyamira Kusini ulipatikana ndani ya kisima kilicho kwenye boma la nyanyake, siku tano baada ya kuripotiwa ametoweka.Mary Arita aliripotiwa kutoweka mnamo Jumanne Machi 29 baada ya kudaiwa kutumwa na nyanyake, ambaye anaishi naye, kuchukua deni kutoka kwa jirani katika kijiji cha Ting’a.

Kulingana na Everline Kwamboka, ambaye anaishi katika boma moja na marehemu, ajuza huyo alimtuma marehemu kuchukua deni kutoka mtaa wa karibu baada ya kutoka shuleni, lakini hakuwahi kuonekana tangu wakati huo. Alisema waliandikisha ripoti katika afisi ya chifu wa eneo hilo siku iliyofuata na pia walitoa ripoti kwa vyombo vya habari vya eneo hilo.

Kwamboka alisema HIYO jana, hisia zake  zilimpeleka kwenye kisima kilichokuwa ndani ya boma hilo, alipokifungua aligundua kuwa kuna kitu kwenye kina cha maji na mara akamuita jirani yake ambaye alishuku kuwa kitu hicho kinaweza kuwa mwili wa binadamu.

Kisha waliitana na kuwavutia wanakijiji. Kaimu Chifu wa eneo hilo aliwaita polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Manga ambao walichukua mwili uliokuwa ukioza kutoka kisimani.Mwalimu mkuu wa Arita, Bw Absolom Ondieki alisema kuwa marehemu alihudhuria shule siku ya Jumanne wiki jana na baadaye hafla ya michezo katika shule jirani na hakuonyesha dalili zozote za mfadhaiko.

Alisema hakufika shuleni siku iliyofuata, jambo lililomfanya kuwatuma wenzake kwenda kumwangalia na baadaye Jumatano mchana, mlezi wake aliripoti shuleni kuhusu kupotea kwake.

 

 

 

April 4, 2023