BY ISAYA BURUGU,4TH FEB,2023-Mwili wa mwanamme aliyezama katika mto Nyamindi katika Kijiji cha Ngucui katika kaunti ya Kirinyaga umoendolewa majini.Mwili huo uliondolewa na wapiga bizi wa kibinafsi na wenyeji waliojitolea.
Kelvin Muthomi ambaye ni mfanyikazi wa hoteli moja mjini Kimbimbi eneo bunge la Mwea alikuwa amekwenda katika mto huo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa na mpenziwe na rafiki alipoteleza na kuanguka majini.
Akizungumza baada ya mwili wa Muthomi kuondolewa majini ,babake marehemu Duncum Mutuma anayetoka kaunti ya Meru amesema alipigwa na mshangao baada ya kupokea ujumbe wa kifo cha mwanawe na akajikaza na kufika eneo la mkasa.
Mutuma ambaye alikuwa ameandamana na jamaa wa familia yake na marafiki anasema ,wapiga bizi walishinda mchana kutwa wakitafuta mwili wa mwanawe hadi mwendo wa saa moja unusu jioni walipofanikiwa kuupata.
Mwili huo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kibugi mjini Kimbimbi ukisubiri upasuaji.