BY ISAYA BURUGU,22ND JUNE,2023-Wabunge hatimaye wamepitisha  ushuru wa nyumba wa kima cha asilimia 1.5 ya mishahara ya wafanyakazi kila mwezi.Katika kura ya moja kwa moja iliyopigwa kwa pendekezo hilo lililowasilishwa na Kamati ya Bunge kuhusu Fedha, wabunge 184 walipiga kura ya NDIO, wengi wao wakiwa wabunge wa Kenya Kwanza.Nao wabunge 72 walipiga kura ya LA kupinga pendekezo hilo linaloungwa mkono na Rais William Ruto.

Kupitishwa kwa ushuru huu usiku wa kuamkia leo sasa kunaashiria kuwa wafanyakazi wote watakuwa wakilipa ushuru wa kima cha asilimia 1.5 kwa mishahara yao kuanzia Julai 1, 2023

Nao waajiri wao watalipa kiasi kama hicho cha mishahara ya wafanyakazi wao kila mwezi.Pesa hizi zitawekwa katika Hazina ya Nyumba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

Ushuru huu, bila shaka utaongeza gharama kwa waajiri hali itakayosababisha baadhi yao kupunguza idadi ya wafanyakazi.

Nao wafanyakazi, ambao tayari wanazongwa na mzigo wa gharama ya maisha, pia watafinyika zaidi na ushuru huu mpya.

 

 

June 22, 2023