Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametangaza kuwa Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Pombe na dawa za Kulevya NACADA itaongezewa fedha ili kuiwezesha kupambana na kero la unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Akizungumza katika eneo la chuka wakati wa mkutano wa kujadili mbinu za kutokomeza kero hilo, Kindiki amedokeza kuwa iwapo fedha hizo zitatolewa basi mamlaka hiyo ya NACADA itahitajika kukaza kamba na kutoa matokeo bora badala ya takwimu za kaunti zinazoongoza kwa utumiaji wa dawa hizo.

June 12, 2023