Raphael Munyua

Naibu Gavana wa Kaunti ya Lamu, Raphael Munyua Ndung’u, amefariki. Taarifa hizi zimedhibitishwa na viongozi wa serikali ambao wameelezea huzuni yao, huku wakituma risala za rambirambi kwa familia yake na wakazi wa kaunti ya Lamu.

Rais William Ruto ameongoza taifa katika kumuomboleza Naibu Gavana huyo, akimtaja kama kiongozi shupavu aliyejitolea kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wa Lamu. Ruto amemtaja marehemu Munyua kama mtu aliyeweka maslahi ya wananchi mbele na kujitahidi kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Viongozi wengine wa kitaifa, akiwemo Naibu Rais Rigathi Gachagua, Waziri Mkuu Musalia Mudavadi, na viongozi wengine wa kisiasa pia wametoa jumbe zao za rambirambi kufuatia kifo cha Naibu Gavana huyo. Wote wameelezea huzuni yao kwa kumpoteza kiongozi mwenye maono na aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa watu wa Lamu.

September 7, 2024