Naibu gavana wa Siaya William Oduol ataendelea kuhudumu kama naibu gavana wa Kaunti hiyo, baada ya maseneta kupinga pendekezo la kumbandua mamlakani lililotolewa na kamati maalum iliyotwikwa jukumu la kuangazia kutimiliwa kwake.
Maseneta 27 wamepiga wakipinga mapendekezo ya kamati hiyo maalum,dhidi ya maseneta 16 waliounga mkono mapendekezo hayo. Kamati Maalum ya bunge la Seneti iliyokuwa ikichunguza kutimuliwa kwa Naibu Gavana huyo ilipendekeza aondolewe afisini kwa madai ya ukiukaji mkubwa wa Katiba na matumizi mabaya ya afisi. Katika ripoti yake iliyowasilishwa mbele ya maseneta hii leo, kamati hiyo ya wanachama 11 ilieleza kuwa baadhi ya madai yaliyotolewa dhidi ya Oduol ni ya kweli hku mengine akiwa hayajadhibitishwa.
Mjadala mkali uliibuka kwenye vikao vya leo kwenye bunge hilo, maseneta wakitoa misimamo tofauti kuhusu ripoti iliyowasilishwa, baadhi ya maseneta wakikosoa uamuzi wa kamati hiyo pamoja na mchakato mzima wa kumbandua ofisini, huku wengine wakitaka kuidhinishwa kwa mapendekezo hayo.