Naibu Rais Rigathi Gachagua hii leo amemwakilisha Rais William Ruto katika toleo la pili la kongamano la Forbes 30 under 30 barani Afrika mjini Gaborone.
Gachagua na mkewe Bi. Dorcas Gachgaua waliondoka nchini leo asubuhi.
Forbes 30 Under 30 inatambua wafanyabiashara bora wachanga wa ubunifu katika sekta za teknologia, Ubunifu, Utamaduni, Michezo, Afya, na Sayansi, kati ya nyanja zingine.
Angalau vijana wanne bora sana wa Kenya walituzwa mwaka wa 2022.
Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Gachagua ameeleza kuwa ni muhimu katika kukabiliana na ukosefu wa ajira katika Bara la Afrika, ambao unakadiriwa kuwa asilimia 12.7pc.
Kando na kuhudhuria kongamano hilo, Naibu rais atakutana na kufanya mazungumzo na Wakenya wanaoishi Botswana.
I left the country this morning for Gaborone, Botswana, to represent our President, H.E @WilliamsRuto, at the second edition of Forbes 30 Under 30 Africa Summit. I am accompanied by my spouse, @Pastor_Dorcas.
Forbes 30 Under 30 recognises outstanding young innovative…
— H.E. Rigathi Gachagua, EGH (@rigathi) April 22, 2023