BY ISAYA BURUGU,28TH NOV,2023-Naibu Rais Rigathi Gachagua ameitaka Idara ya Mahakama kuzingatia athari pana kwa jamii kutokana na uamuzi wake wa kutangaza ushuru wa nyumba kuwa kinyume na katiba.

Akizungumza hivi leo  alipofungua rasmi Kongamano la 17 la kila mwaka la Taasisi ya Mipango ya Kenya katika Kaunti ya Kwale, Gachagua aliangazia kuwa licha ya kuongezwa ushuru kwa walipa ushuru, ushuru huo unawezesha serikali kujenga nyumba kwa wingi ili kupunguza uhaba wa makazi nchini Kenya.

Aliongeza kuwa utawala wa Kenya Kwanza umejitolea kutekeleza ajenda ya makazi ya gharama nafuu kwa kujenga nyumba 250,000 kila mwaka, licha ya vikwazo vya kisheria vinavyoletwa na baadhi ya walalamishi kupinga mpango huo.

.Maoni ya DP Gachagua yanakuja baada ya Mahakama Kuu jijini Nairobi kutangaza ushuru huo wa nyumba kuwa kinyume na katiba kwamba unakiuka Kifungu cha 10, 2 (a) cha katiba.

 

 

November 28, 2023