Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema kuwa hivi karibuni atabuni kamati ya washikadau mbalimbali itakayojumuisha magavana wa ukanda wa pwani ili kujadili mbinu za kukabili uraibu wa dawa za kulevya katika ukanda huo.

Akizungumza katika kaunti ya kilifi, Gachagua ameeleza kuwa uraibu na uuzaji wa dawa hizo umekithiri katika eneo hilo hali inayowaharibia maiha vijana wengi huku akiwaomba viongozi wa dini kuingilia kati pia na kuwapa ushauri nasaha vijana katika ukanda huo.

Kuhusiana na suala la elimu, Gachagua amesema kuwa serikali itaendelea kusaidia taasisi za elimu nchini  kwa matokeo bora.

Gachagua aliandamana na Gavana Gideon Mung’aro (Kaunti ya Kilifi), Owen Baya (Mbunge wa Kilifi Kaskazini), Katibu wa Baraza la Mawaziri Salim Mvurya (Uchumi wa Madini na Bluu), Lydia Haika, (Mwakilishi wa Wanawake Taita Taveta), Rahab Mukami, (Mwakilishi wa Mwanamke Nyeri ), Vincent Kawaya, (Mbunge wa Mwala), Onesmus Ngoyoyo (Kajiado Kaskazini), Muthoni Marubu (Mwakilishi wa Wanawake wa Lamu), Maryanne Keitanny (Mbunge wa Aldai), Mohamed Ali (Mbunge wa Nyali), Muiruri Stanley (Mbunge wa Lamu Magharibi), Anthony Kenga ( Mbunge wa Rabai), Hillary Kosgei (Mbunge Kipkelion Magharibi), Joseph Cherorot (Mbunge wa Kipkelion Mashariki), John Kaguchia (Mbunge wa Mukurweini), Kamau Murango (Seneta wa Kirinyaga), Danson Mungatana (Seneta wa Tana River), miongoni mwa wengine.

November 11, 2023