Nchi 26 za Afrika zilipiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kupinga kura za maoni zenye utata wa Moscow katika mikoa minne ya Ukraine ambayo ilitangaza kuwa ni sehemu ya Urusi.
Nchi 19 hazikupiga kura hiyo, ikiwa ni pamoja na Eritrea ambayo hapo awali ilipiga kura ya kukataa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Nchi zinazodhaniwa kuwa washirika wa Russia ni zikiwemo Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia, Jamhuri ya Kongo, Afrika Kusini, Sudan, Uganda na Zimbabwe.
Nchi tatu kati ya hizi zilimkaribisha mwanadiplomasia mkuu wa Urusi Sergei Lavrov alipozuru bara la Afrika mwezi Julai. Burkina Faso, Kamerun, Guinea ya Ikweta na Sao Tome hazikuwepo katika kusanyiko hilo.
Mapema mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alizuru barani Afrika kukabiliana na Urusi inayoonekana kushikilia bara hilo na kuwashawishi viongozi kuunga mkono Kyiv.Alilazimika kukatiza ziara hiyo baada ya Moscow kuzidisha mashambulizi dhidi ya Ukraine.