Bodi ya Kitaifa ya Mazao na Uhifadhi wa Nafaka nchini (NCPB) imefungua maghala yake kwa lengo la kutoa fursa kwa wakulima kuweza kuhifadhi mazao yao kwa njia bora na kuepuka hasara zinazoweza kutokea kutokana na uhifadhi duni wa mazao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NCPB Bwana Joseph Kimote, amewataka wakulima na wauzaji wa nafaka kuchangamkia huduma za uhifadhi zinazotolewa na bodi hiyo kwa manufaa yao. Bwana Kimote ameeleza kuwa NCPB itawasaidia wakulima kufurahia mazao yao kwa kuwapa huduma za kukausha na kuhifadhi nafaka zao, pamoja na kufanya vipimo vya uwepo wa sumu ya Aflatoxin.
SOMA PIA: Linturi awaomba wakulima Narok kuuza mahindi yao ili kuepuka hasara.
Aidha, amethibitisha kwamba huduma za kukausha nafaka zitapatikana katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na Nairobi, Eldoret, Kilgoris, Nakuru, Narok, Kisumu, Moi’s Bridge, Kitale, na Bungoma.NCPB imeeleza kwamba asilimia 30 ya mazao yote yanayozaliwa humu nchini kila mwaka hupotea kutokana na uhifadhi usiofaa wa mazao.
Affordable Grain Post-Harvest services available at NCPB… pic.twitter.com/e9xAEVeN7T
— National Cereals & Produce Board (@NCPB_KE) October 24, 2023