Miaka mitano baada ya mamlaka ya utunzaji mazingira nchini NEMA kufutilia mbali matumizi ya karatasi za plaski kutokana na madhara yake, baadhi ya wananchi wameanza kurejelea tena utumizi wa karatasi hizo wengi wakisemekana kuwa wafanyabiashara katika maeneo ya soko.
Ni hali ambayo imepelekea maafisa kutoka NEMA kuendeleza oparesheni ya kuwanasa wanaotumia karatasi hizo katika soko la ololulunga.
Kwa mujibu wa afisa wa mamlaka ya NEMA Salome Machwaa ni kwamba walifanikiwa kuwanasa watu 7 ambao walipatikana wakikaidi sheria za NEMA.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa mamlaka hiyo tawi la Narok fanuel masago ameshikilia kwamba oparesheni ya kuwanasa wale ambao bado wanatumia karatasi za plastiki inaendelea na akisisitiza kuwa wanaangazia pakubwa maeneo yanayopakana na mbuga ya kitaifa ya wanyama pori ya maasai mara kwa ajili ya usalama wa wanyama kwenye mbuga hiyo.
NEMA today arrested 7 traders from Ololulunga Market with banned plastics bags. The traders will appear in court. NEMA appeals to all markets countrywide to desist using banned plastic bags and any offender found guilty risks a fine of not less than 2m or 6 months jail term. pic.twitter.com/QvufzWAsPO
— NEMA Kenya (@NemaKenya) January 17, 2023