Tukisalia katika taarifa zenye uzito sawia kuhusiana na maandamano ya hio jana, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Nordin Haji amemwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome kuanzisha uchunguzi kubaini sababu za matukio ya ghasia yaliyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya mrengo wa upinzani dhidi ya serikali yaliyoandaliwa siku ya jana.
Katika waraka wake kwa inspekta jenerali, Bwana Haji alieleza kwamba vitendo vya mauaji, uteketezaji wa majumba na vitu vingine, vitendo vya unyanyasaji na uharibifu ni kinyume cha sheria hivyo ni lazima wahusika wafikishwe mahakamani.
Ofisi ya DPP imemwagiza inspekta Jenerali kukamilisha uchunguzi wake katika kipindi cha siku 14 zijazo, huku wakieleza kujitolea kwao kulinda haki za wakenya, na kuhakikisha kwamba wahalifu wote wanakabiliwa kisheria.