BY ISAYA BURUGU,14TH JUNE,2023-Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Haji ameapishwa rasmi kama mkurugenzi wa idara ya kijasusi nchini NIS.Kuapishwa kwake kunajiri siku moja baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha uteuzi wake.

Haji anachukua hatamu kufuatia kustaafu kwa Meja generali Philip Wachira Kameru aliyestaafu mwaka mmoja kabla ya kipindi chake kukamilika rasmi.Hafla ya Kuapishwa kwa Noordin Haji imeongozwa na rais  Wiliam Ruto  katika Ikulu ya Nairobi

.

Kwa upande wake rais Ruto amemtaka Haji kutekeleza wajibu wake mpya kwa uadilifu  na kufahamu kuwa idara ya kijasusi ni muhimu kwa ustawi wa kitaiafa Rais akiongeza kuwa ni sharti Haji atekeleze jukumu lake vyema Zaidi ikizingatiwa kuwa mstakabali wan chi kwa sasa na siku zijazo unategemea idara hiyo

 

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mawaziri, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi miongoni mwa maafisa wengine wakuu.

Kabla ya kuwa DPP, Haji aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kukabiliana na Uhalifu uliopangwa ndani ya Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi.

 

 

 

June 14, 2023