BY ISAYA BURUGU ,10TH APRIL,2023-Chama cha ODM kimepuzilia mbali taarifa kuwa kimewabadilisha viongozi wa chama hicho katika kaunti ya Kakamega.Kupitia taarifa iliyotolewa leo,Chama hicho kimedai kuwa kimepokea taarifa zinazodai kuwa kumekuwa na mageuzi ya uongozi wa chama katika kaunti hiyo.
ODM ikizitaja ripoti hizo kama zakupotosha ,a kusema kuwa hakuna uchaguzi ua mabadiliko ya viongozi yatakayofanywa bila bodi yakitaifa ya chama hicho kutoa idhini kama inavyohitajika kisheria.
Wameweka bayana kuwa mabadiliko katika uongozi wa chama ni sharti yapitie katika uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa baadaye mwaka huu .
Chama hicho kimesema kuwa walio na nia ya kujiuzulu ni sharti wafuate utaratibu uliyoko.Wakati huo huo walio na nia ya kuwania nafasi mbali mbali chamani huo wameshauriwa kuanza kujifahamisha na kanuni zinazosimamia uchaguzi wa mashinani kusubiri tarehe ya uchaguzi wenywe.