Mzozo unaoshuhudiwa kati ya idara ya mahakama na viongozi wakuu serikalini umechukua mkondo tofauti baada ya kuwasilishwa kwa ombi la kutaka kuondolewa ofisini kwa Jaji Mkuu Martha Koome.
Ombi hilo limepelekwa kwa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) na Michael Kojo Otieno, anayemtuhumu Jaji Mkuu kuhusika katika shughuli za ufisadi.
Kojo amedai katika ombi lake kwamba Jaji Mkuu hakuifuata sheria katika uteuzi wa wajumbe wa Jopo la kuangazia upya masuala ya ushuru nchini. Pia, amemtuhumu Jaji Mkuu kwa ubaguzi na kutowafuata kanuni za kisheria katika utendakazi wake. Haya yote yanadaiwa kuwa sababu za kutosha za kumtaka Koome aondoke ofisini.
SOMA PIA :Jaji Mkuu Akutana na Rais Kutatua Uhasama Kati ya Serikali na Idara ya Mahakama.
Ombi hili limekuja siku chache baada ya kikao kati ya Rais William Ruto na Jaji Mkuu Martha Koome. Kikao hicho kilifuatwa na maamuzi ya mahakama ambayo yamesitisha mipango miwili ya serikali. Maamuzi hayo ni pamoja na kusitisha ukusanyaji wa ushuru wa ujenzi wa nyumba na mpango wa kuwatuma maafisa wa polisi haiti.