Ombi limewasilishwa mahakamani la kutaka kuwazuia Cleophas Malala, David Ndii, Monica Juma na Harriette Chiggai kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri.
Mlalamishi, Charles Mugabe anasema kuwa uamuzi wa kuwaruhusu wanne hao kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri ni kinyume cha katiba.
Aidha anadai kuwa wanne hao waliapishwa kwa usiri katika Ikulu ya Nairobi kabla ya kuhudhuria mkutano wao wa kwanza.
Mugabe anasema kuendelea kwao kuhudhuria mikutano ya baraza hilo kunazua maswali mazito ya Kikatiba ambayo mahakama inapaswa kuyashughulikia mapema.
Rais William Ruto aliwaidhinisha wanne hao kuhudhuria vikao vya baraza hilo licha ya matakwa ya Kifungu cha 152 kwamba wanachama wa Baraza la Mawaziri wawe Rais, Naibu Rais, Mwanasheria Mkuu na Mawaziri kati ya 14 na 22.