Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ameeleza kuwa oparesheni ya maliza uhalifu inayoendeshwa katika kaunti sita zilizoko eneo la kaskazini mwa bonde la ufa inendelea vyema.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufuzu kwa maafisa wa akiba katika eneo la Kimalel kaunti ya Baringo, Kindiki amedokeza kuwa timu inayoendesha oparesheni hiyo imefanikiwa kuwatoa mafichoni wahalifu ambao wamekuwa wakiwahangahisha wakaazi wa kaunti hizo.

Ameongeza kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2023, kila Askari wa  akiba atakuwa na bima ya matibabu ya NHIF. Hii itapanuliwa kwa wanafamilia wao.

Hali kadhalika ameeleza kuwa sare ya NPR unakaribia kukamilika ili  kuwawezesha maafisa hao kutekeleza majukumu yao.

Mgao wa awali wa Ksh.100M umetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule zote ambazo ziliharibiwa na majambazi. Maafisa wa KDF watasimamia ujenzi huo. Ksh.100M nyingine itatolewa katika awamu ya pili ili kukamilisha ujenzi huo.

Serikali pia itaajiri  walimu 100 wa ziada; 50 wataenda Baringo Kusini na 50 Baringo Kaskazini kuhakikisha masomo katika shule zilizofunguliwa yanaendelea bila kukatizwa.

May 18, 2023