Asasi za usalama zinazo ongoza operesheni katika maeneo ya kaskazini mwa bonde la Ufa, zimefanikiwa kutwaa bunduki 96 kutoka kwa wahalifu wanaoiba mifugo katika kaunti ya Samburu.
Bunduki hizo zikiwemo zile za aina ya M16 zimetwaliwa katika kipindi cha wiki tatu. Aidha mbuzi 72 waliokuwa wameibwa na wahalifu hao wamerejeshwa huku maafisa wa usalama wakiendelea kuwasaka mifugo wengine 169 na bunduki mbili ambazo majangili walitoweka nazo.
Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amekutana na maafisa wakuu wa usalama wa bonde la ufa kukagua jinsi oparesheni ya maliza uhalifu inavyoendelea. Waziri huyo amesema kwamba makamishena wa kaunti zote watahusika moja kwa moja katika kuwakabili wahalifu wanaoiba mifugo.