BY ISASYA BURUGU,4TH JULY,2023-Polisi walilazimika kufyatua vitoa machozi kuyatenganisha makundi mawili hasimu katika mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa kundi jipya la hifadhi ya mbuga ya Mara Ripoi ,wadi ya Siana Narok Magharibi kufuatia mzozo wa uongozi.Vurumai ilianza baada ya mwanachama anayedaiwa kutoka kundi la kamati shikilizi kunyakua kipasa sauti kwa nguvu kutoka kwa muongoza ratiba na ndiposa makabiliano yakaanza.Zaidi ya wanachama 2000 walikuwa wamehudhuria mkutano huo.
Wafuasi wa kundi hilo linaoegemea upande wa mwakilishi wadi hawakuachwa nyuma kwani walifurika wakiwa wamejihami tayari kukabiliana na hali yoyote.Katika purukushani hiyo, baadhi ya vijana wamoran walionekana wakimtisha kwa karibu afisa wa polisi aliyedaiwa kufyatua risasi wakimuonya kutorudia tena.Kwa bahati nzuri Buru Dida naibu mpya wa kamishna eneo hilo kwa ushirikiano na polisi walifanikiwa kushusha joto kati ya pande hizo mbili na kurejesha utulivu.
.Katika mkutano huo maafisa walioteuliwa kushikilia ofisi kwa muda wanadaiwa kuidhinishwa rasmi kama viongozi na afisi kuu ya uhifadhi wa mbuga ya Wanyama pori Maasai Mara.Hatua HIYO iliyopingwa vikali na kundi linaoongozwa na mwakilishi wadi wa Siana Moses Sikona wanaosisitiza kufanyika kwa uchaguiz kuwachagua maafisa wapaya kwa njia ya wazi na kidemokrasia.
.Hifadhi ya Mara Ripoi ni ya hekari 30,000, iliyozinduliwa mwaka wa 2008 na inajivunia aina ya mmbwa mwitu pamoja na paka wa aina yake ambao hawapatikani kwingineko miongoni mwa wanyama pori wengine.