Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametangaza kuanzishwa kwa jimbo jipya katika eneo la Wote, kaunti ya Makueni. Hatua hii ya kihistoria inalenga kuimarisha huduma za kiroho na kuwahudumia waumini katika eneo hilo kwa njia bora zaidi.
Tangazo hilo limetolewa na mwakilishi wa Papa Francis nchini Kenya na Sudan Kusini, Askofu Mkuu Hubertus Matheus Maria Van Megen, ambaye alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kutiliwa maanani kilio cha waumini wengi kutoka kaunti ya Makueni. Changamoto za kiroho na mahitaji ya waumini katika eneo hilo yamewezesha kuanzishwa kwa jimbo jipya ili kuhakikisha kuwa huduma za kiroho zinawafikia kwa ukaribu zaidi.
Kwa muda mrefu, waumini wa kaunti ya Makueni wamekuwa wakihitaji uongozi wa kiroho unaofaa na huduma bora za kanisa. Kuanzishwa kwa jimbo jipya la Wote kutatenganisha eneo hili kutoka Jimbo Katoliki la Machakos na kutoa nafasi ya kuwa na uongozi wa karibu na makini zaidi.
Mara baada ya tangazo hilo, Papa Francis pia amemteua Askofu Paul Kariuki Njiru kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo hilo jipya la Wote. Askofu Paul Kariuki Njiru amepokea uteuzi huo kwa furaha na amejitolea kutoa huduma yake kwa jili ya kusaidia ukuaji wa kiroho na maendeleo ya jamii katika eneo hilo jipya.
Pope Francis has appointed Rt. Rev. Paul Kariuki Njiru, bishop of the Catholic Diocese of Embu as the new bishop of newly erected Catholic Diocese of Wote, the Holy See Press Office has announced.
— The Seed Magazine (@MagazineSeed) July 22, 2023
KUKMHUSU ASKOFU PAUL KARIUKI NJIRU