BY ISAYA BURUGU 3RD AUG 2023-Papa mtakatifu Francis amewataka vijana kutilia maanani utunzaji wa dunia na mabadiliko ya hali ya Anga akitaja kama kiungo muhimu kinachohitaji kulindwa kwa kupigana na umaskini na chagamoto zingine za kijamii.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 86 amefanya utunzjai wa mazingira lengo lake kupitia nyayo yake ya “Laudato Si” inayo taka kila juhudi kuelekezwa katika utunzaji wa mazingira.
Papa amesema hayo wakati akiwahutubia Zaidi ya wanafuzni 6500 katika chuo kikuu katoliki cha Lisbon katika siku yake ya pili ya ziara yake nchini ureno.
Papa aliwasili mjini Lisbon jana jumatano kuhudhuria hafla ya siku ya vijana duniani ambayo ni sherehe ya wiki moja ya kimataifa ya kikatoliki inayotarajiwa kuwavutia watu milioni moja.