BY ISAYA BURUGU 15TH MAY 2023-Mhubiri Ezekiel Odero wa new life Church katika kaunti ya Kilifi amepata pigo jipya baada ya mahakama kuu jijini Mombasa kukataa ombi  kutoka kwa mhubiri  huyo  lililoitaka kuagiza akaunti zake za benki na kituo cha televisheni kufunguliwa.

Jaji wa makahama   Olga Sewe  amesema ombi hilo halikufaa kwa wakati huu na hivyo basi agizo lililotolewa na mahakama ya hakimu jijini Nairobi kuhusu akaunti hizo  na kituo chake cha Runinga linasalia.

Mahakama imepuzilia mbali ombi la kutaka leseni ya televisheni ya mhubiri huyo kurejeshwa ikisema Odero alipaswa kushughulikia maswala yote yakisheria na tume ya mawasiliano nchini kabla ya kufika mahakamani

Odero anatuhumiwa kuwa na uhusiano na dhehebu potovu lililopelekea watu wengi kuaga dunia kutokana na kufunga kula katika msitu wa Shakahola.

Alikamatwa kufuatia kuzuiliwa kwa kiongozi wa dhehebu potovu la Goodnewss International Church kule Kilifi.

Hadi kufikia sasa miili 210 imefukuliwa kutoka makaburi ya alaiki msituni humo.

 

.

 

May 15, 2023