Jamii ya Abagusii, ni kabila la Wabantu ambao wanaishi katika Kaunti ya Kisii kusini-magharibi mwa Kenya. Jamii ya Abagusii ni mojawapo ya jamii zenye idadi kubwa sana ya watu katika taifa la Kenya. Katika ramani ya taifa la Kenya, jamii ya Abagusii inapatikana kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya Kaskazini magharibi na huunganishwa na ukanda wa Nyanza mara kwa mara.

Wao ndio kabila kubwa zaidi katika Kaunti ya Kisii, na lugha yao, ambayo pia huitwa Kisii au Ekegusii, ni lahaja ya familia ya lugha ya Kibantu. Wanajamii wa Abagusii kama tu jamii nyingi humu nchini, wanaamini kwamba chimbuko lao lilikuwa nje ya taifa la Kenya, kabla yao kuwasili humu nchini miaka ya kale na kisha kujinyakulia mahala pao wanapoishi.

Sikiliza makala haya uanze safari yako ya kuifahamu jamii hii, pamoja na mila, itikadi, tamaduni na pia desturi zao.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

 

May 5, 2023

Leave a Comment