Mwongozo wa desturi za Abagusii uliheshimu sana familia kama kituo cha muhimu Zaidi katika jamii, huku wanaume wakiwa na uwezo wa kuoa Zaidi ya mke mmoja. Kutokana na kiwango kikubwa cha heshima kati ya wanaume na wanawake, mke wa kwanza alikuwa na jukumu la kumtafuta mke wa pili kwa mumewe na kumleta kwenye boma lao. Mke huyu mdogo alimheshimu mke mkubwa kwa kila hali na alichukuliwa kama mmoja wa familia hii, akipewa heshima na mumewe na pia wanajamii wengine.

Taasubi za kiume pia zilishuhudiwa kwa kiwango kikubwa katika tamaduni za jamii hii, kwani kila mwanaume alikuwa na Fahari kuwa na Watoto wa kiume, ambao wangesaidia katika kulinda rasilimali za jamii, na pia kuendeleza tamaduni za familia. Watoto wa kike kwa upande mwingine nao walionekana kama ishara ya utajiri na ukwasi kwa familia, kwani familia iliyokuwa na wana wengi wa kike ilipata kupata mifugo wengi kutokana na mahari iliyoletwa wakati wana wale walifikia umri wa kuolewa.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

May 17, 2023

Leave a Comment