Katika mila na desturi za jamii ya wamaasai,  kulikua na mfumo wa kutofautisha watu wa jinsia moja na ile nyingine, mtindo wa mavazi na majukumu yao katika jamii yakiwa vigezo vikubwa vya kufanikisha haya. Katika jamii, mambo kadhaa yalitengewa wanaume, baadhi yakitengewa wanawake na mengine kutekelezwa na wanajamii kwa pamoja.

Uwezo wa wanawake katika jamii hii, ulidunishwa sana, kwani jamii ya wamaasai iliwainua wanaume zaidi na hivyo kuwaona wanawake kama wasio na uwezo wa kuwa viongozi katika jamii hiyo, hivyo basi wanawake hawakuwa na uwezo wa kutwaa nyadhifa zozote za uongozi na pia walitengwa katika baadhi ya vikao kama vile kupanga vita au mipango ya kuvamia jamii zingine kwa nia ya kutwaa mifugo au Raiding kwa lugha ya kiingereza, shughuli ambayo ilitekelezwa na wanaume.

Kwa malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi.

October 27, 2022

Leave a Comment