Baada ya wazazi kuwaunganisha mvulana na msichana wanaopaswa kuoana na kuhakikisha kwamba wamejuana, wazee kutoka upande wa mvulana walianza mchakato wa kuelekea katika aila ya binti anayeozwa ili kujitambulisha rasmi na kuanza mazungumzo ya kuunganisha familia hizi mbili. Shughuli hii ilikuwa mwanzo wa msururu wa shughuli nyingi za sherehe ya harusi iliyotambulika kama Oboko.
Ili kuhakikisha kwamba posa lako limekubalika, upande wa aila ya mvulana anayetafuta mke walipaswa kupeleka mbuzi wanne kwa boma la binti huyu,kwa kufuata mfumo maalum. Mbuzi wawili kati ya wanne waliopelekwa walipaswa kuliwa katika hafla ya kuzikutanisha familia hizi mbili, na kisha kuendelea kwa sherehe hii ya harusi hadi tamati. Mbuzi waliosalia kati ya wale wannne waliopelekwa kwa boma la binti anayeolewa walipaswa kuchinjwa na kurejeshwa katika boma la mvulana wakiandamana na ugali wa wimbi, ambao ulikuwa ishara ya kusimika mahusiano kati ya familia hizi mbili.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke