Vijana wa kimaasai walipofikia umri Fulani, walianza kutuma ujumbe kwa wazee katika jamii kuwa wanafaa kukaribishwa ukubwani. Haya waliweza kuyafanya kwa kutwaa baadhi ya majukumu yaliyoonekana kuwa ya watu wazma na kuanza kuyatekeleza.

Majukumu haya yalijumuisha mambo kama vile kuwapeleka Mifugo malishoni hasa nyakati za kiangazi, uwindaji wa Wanyama pori na vilevile maswala ya ulinzi wa jamii. Baadhi ya mambo mengine ambayo vijana hawa walipaswa kutekeleza, yalitokana na mafunzo waliyopokea au kwa kutazama yale wazee na wanaume wengine katika jamii hii walikua wakitenda.

Mafunzo haya yalikua kiungo muhimu sana kwao kabla ya kupashwa tohara, kwani walifaa kuyategemea katika Maisha yao ya baadaye. Kuwatibu au hata Kuwachinja Wanyama, kuunda silaha Pamoja na kujua jinsi vipande vya nyama vilifaa kutolewa na makuni yaliyofaa kula vipande hivi, jambo ambalo lilifanywa kwa umakini mkubwa kwani kulikua na malipizi kwa lolote linaloenda mrama.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

January 11, 2023

Leave a Comment