Jukumu la malezi ya Watoto katika tamaduni na jamii ya kimaasai, lilikua jukumu la wanajamii wote, kuanzia kwa wazazi wa mtoto, jamaa wa karibu, Watoto wenzake na hata jamii nzima kwa ujumla.
Katika siku ya kupewa jina kwa mtoto, familia ya mtoto ilitafuta msimamizi wa mwana wao, aliyekuwa wa jinsia moja na mtoto mwenyewe aliyefaa kutoka katika familia au ukoo tofauti na mtoto mwenyewe. Msimamizi huyu alifaa kuwa mtu mwenye maadili mema na aliyekuwa…
Ili kuwa na kizazi cha siku za usoni, Watoto huwa kiungo muhimu katika kila jamii. Katika jamii ya kimaasai, Watoto walianza kulindwa wakiwa katika tumbo la mama, na hivyo kina mama wajawazito waliangaziwa kwa njia tofauti wakilinganishwa na wanajamii wengine. Baada ya…
Uwezo wa wanawake katika jamii hii, ulidunishwa sana, kwani jamii ya wamaasai iliwainua wanaume zaidi na hivyo kuwaona wanawake kama wasio na uwezo wa kuwa viongozi
Chanzo cha kila jamii kote ulimwenguni huwa Familia. Ni kutokana na familia ndipo tunapata jamii na hata taifa. Katika awamu ya leo, tunaangazia muundo wa familia ya Kimaasai
Sikiliza makala haya ili upate kuelewa bayana kuhusu Chimbuko la Jamii ya Maasai na jinsi walifika katika taifa la Kenya na maeneo mengine wanakopatikana.